33% ya vifo nchini vinatokana na magonjwa yasiyoambukiza

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,430
8,244
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA), Profesa Andrew Swai amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kusababisha vifo vingi nchini ikilinganishwa na miaka ya 1980.

Kutokana na ongezeko hilo, Serikali imetangaza mpango wa kuanza kuwapima wananchi wanaokwenda kupata huduma za Afya na itaanza na wanaopata huduma za mama na mtoto pamoja na wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

Profesa Swai amesema magonjwa hayo yanaathiri hasa watu wenye umri mdogo wakiwamo watoto ambapo wengi wanakufa kabla ya hawajafika hata miaka 70.
 
Back
Top Bottom