Watanzania takriban milioni 22 sawa na asilimia 52 wanaugua ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Watanzania takribani milioni 22 sawa na asilimia 52 wanaugua ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo,Kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 50 hadi 80 ya magonjwa hayo yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTD) Mkoa wa Mwanza, Dkt. Mabai Leonard, alisema kuwa ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo bado ni tatizo kubwa mkoani humu.

Dkt.Mabai alisema kuwa, takribani Watanzania milioni 22 wanaugua kichocho na minyoo ya tumbo, ili kukabiliana na tatizo hilo Mkoa wa Mwanza umeandaa zoezi la utoaji wa kingatiba kwa watoto wa umri wa kwenda shule kuanzia miaka 4 hadi miaka 15 wa shule za msingi zote ambapo sh. 288,474,400 zimetengwa kwa ajili ya zoezi hilo.

Aidha,aliongeza kuwa ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo hauna dalili za haraka kabla ya kupata matibabu hivyo zoezi la kutoa kingatiba inalenga kudhibiti na kutibu magonjwa hayo kwenye jamii.

Hata hivyo alisisitiza kuwa, halmashauri zote mkoani Mwanza zihakikishe watoto watakaopewa kingatiba wamepata chakula saa mbili kabla ya kumeza alizitaja Kingatiba hizo ni aina ya Albendazole kwa ajili ya minyoo ya tumbo na Prazequantel ya kichocho.

"Tatizo la ugongwa wa kichocho na minyoo ya tumbo mkoani Mwanza linasababishwa na jiografia yake ya kuwa na maji mengi, shughuli za kilimo (majaruba ya mpunga) asili ya madimbwi ya maji na hivyo wananchi wako kwenye hatari ya kupata magonjwa hayo," alisema Dkt.Mabai.

Naye Profesa Huphrey Mazigo wa Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi na Tiba za Afya Bugando(CUHAS), alisema magonjwa 17 yakiwemo kichocho na minyoo yaliyo Ukanda wa Tropiki yanaikumba jamii masikini vijijini hasa zinazoishi chini ya Dola 2 na zisizo na uwezo wa kugharamia tiba na athari kwa watoto wa umri wa kwenda shule.

“Tanzania ni moja ya nchi zilizoathiriwa na ugonjwa wa kichocho hasa bonde la Ziwa Victoria hasa wakulima, wavuvi na watoto na watu bilioni 2 duniani wameathirika na minyoo ya tumbo, zaidi ya watu milioni 300 wameathirika sana huku 155,000 kila mwaka duniani hufariki kutokana na magonjwa hayo,”alisema Profesa Mazigo.


Michuzi Blog
 
... miongoni mwa indicators of absolute poverty ni magonjwa dizaini hiyo - kichocho, kuhara, UTI, upofu, ukoma, etc. ambayo hutokana na huduma mbovu za jamii - maji, elimu, afya, matundu ya vyoo, makazi duni, n.k! Lack of very basic needs, education, and skills. Anyway, hizi mambo ndizo hupelekea ushindi wa kimbunga; ndio "uchawi wetu huu"!
 
... miongoni mwa indicators of absolute poverty ni magonjwa dizaini hiyo - kichocho, kuhara, UTI, upofu, ukoma, etc. ambayo hutokana na huduma mbovu za jamii - maji, elimu, afya, matundu ya vyoo, makazi duni, n.k! Lack of very basic needs, education, and skills. Anyway, hizi mambo ndizo hupelekea ushindi wa kimbunga; ndio "uchawi wetu huu"!
Sawa bwana tumewasiliana nyie wataalamulakini sie ni matajiri, na huo ni wivu wa mabeberu' kwa kuwa tuko uchumi wa kati... kazi iendelee.
 
Watu milioni 22 kuwa sawa na 52% ya Watanzania kwa takwimu za wapi.....
(Tanzania / Population
58.01 million (2019)
Source: World Bank)

 
Back
Top Bottom