Mlima Kilimanjaro umepoteza 90% ya barafu kwa miaka mia iliyopita

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
Mlima Kilimanjaro, uliopo nchini Tanzania umepoteza asilimia 90 ya barafu yake katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, kwa mujibu wa wanasayansi.

Mlima huo mrefu kuliko yote Afrika, ukiwa na mita 5,895 ni mmoja kati ya milima mirefu Afrika Mashariki inayopoteza barafu.

Wanasayansi hao akiwemo Profesa Clavery Tungaraza wa Tanzania na Dk Doug Hardy kutoka Marekani mbaye alikuwa miongoni mwa wanasayansi wa kwanza kabisa kufanya utafiti mlima Kilimanjaro, wamesema kama hatua hazitachukuliwa huenda barafu ikatoweka kabisa katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Simon Mtuy amepanda mlima Kilimanjaro mara nyingi na familia yake imekuwa ikilima katika miteremko ya mlima huo kwa karnekadhaa sasa, ameiambia BBC kuwa katika maisha yake ameshuhudia mabadilikomakubwa katika mlima huo na hali ya hewa.

BBC Swahili
 
Wasomi wa bungeni watapendekeza zifungwe freezer za kisasa juu ya kilele
 
Back
Top Bottom