Iringa: Ajinyonga baada ya kuzidiwa na Madeni ya VICOBA

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,283
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Enea Mkimbo (55) Mkazi wa Kihesa Kilolo Manispaa ya Iringa, amejinyonga leo September 14, 2022 chanzo kikidaiwa kuwa ni kuzidiwa na madeni ya VICOBA na usumbufu kutoka kwa wanakikundi wenzie.

Mwenyekiti wa mtaa huo Michael Mlalwe amesema marehemu Enea ambaye ameacha mume na watoto watano, jana September 13, 2022 alifuatwa na wanakikundi wakimshinikiza kutoa pesa, ambapo baada ya tukio hilo Enea alimuaga mumewe kuwa anaenda kulala kwa mama yake mzazi eneo la Ilembila na badala yake aliingia jikoni na kujinyonga kwa kutumia kitenge.

Mwenyekiti huyo amesema serikali ya mtaa inapanga kuwaita wanakikundi ili kujua walizungumza nini na Enea mpaka kufikia hatua ya kujitoa uhai wake.

Kufuatia tukio hilo wananchi wa mtaa huo wameiomba serikali kuangalia upya uwepo wa taasisi zinazotoa mikopo kwa riba kubwa inayoumiza wananchi maarufu kama mikopo ya moto ambayo imekua ikichangia watu kujitoa uhai.

Millard Ayo
 
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Enea Mkimbo (55) Mkazi wa Kihesa Kilolo Manispaa ya Iringa, amejinyonga leo September 14, 2022 chanzo kikidaiwa kuwa ni kuzidiwa na madeni ya VICOBA na usumbufu kutoka kwa wanakikundi wenzie.
Vikoba vinavunja ndoa za watu, vikoba vinasababisha watu kukimbia familia zao, vikoba vinasabisha mtu kuishi maisha ya kujificha, vikoba vimesababisha kuuzwa kwa vitu vya ndani; makochi, TV.
 
Visa vya watu kujiua kisa vicoba inazidi kuongezeka kila siku.!

Maisha yamekua magumu mno, biashara haziendi na tozo kila kona.! Mungu tusaidie
 
Visa vya watu kujiua kisa vicoba inazidi kuongezeka kila siku.!

Maisha yamekua magumu mno, biashara haziendi na tozo kila kona.! Mungu tusaidie
Ukiangalia kwa undani utagundua hata ambao hawajihusishi na vicoba na wao hali ni hii hii, inawezekana ugumu wa maisha unakua kwa kasi, na wala hakuna njia mbadala za kuutatua.
 
Mwenyezi Mungu amrehemu na ajalie pumziko la amani, kama haujawahi kuwa na mikopo kwenye vitaasisi hivi vidogo vidogo huwezi ku experience hali alio kua nayo marehemu kabla ya kufariki kwake.
Binafsi sita sahau 2008 na sitawasahau pride na finca.
 
Back
Top Bottom