Wizara ya Kilimo: Tanzania haijavamiwa na Nzige

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1581326752720.png

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet N.Hasunga (MB) jana Jumapili anawafahamisha wakulima na wananchi kwa ujumla kuwa taarifa zinazoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa nzige wa Jangwani nchini hususan mkoa wa Kilimanjaro siyo za kweli.

Mhe.Hasunga amesema hayo wakati alipoongea na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1) na kusema “ hakuna taarifa za kitaalam zilizothibitisha uwepo wa nzige kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Ila ni kweli Kuna nzige wameonekana Kaunti ya Kajiado nchini Kenya takribani kilomita 50 toka mpakani na Tanzania” alisema Waziri wa Kilimo

Wataalam wa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo duniani (FAO) linaendelea na ufuatiliaji wa viashiria vya uwepo wa nzige na tayari hatua za awali za kuwadhibiti endapo wataingia nchini zimechukuliwa. Hatua hizo ni pamoja na Mashirika ya kimataifa ambayo sisi ni wanachama kutuahidi ndege tatu maalum za kunyunyizia dawa na uwepo wa dawa za tahadhali kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Wizara inatoa wito kwa wakulima, maafisa ugani na kilimo na wadau wote wa kilimo kuendelea kutoa ushirikiano wa taarifa sahihi kwa serikali endapo kutajitokeza viashiria vya nzige kwenye maeneo ya mashamba.

Aidha,vyombo vya habari vinasisitizwa kutoa taarifa sahihi na za ukweli ili kuepusha sintofahamu kwa wakulima.

Imetolewa na;
Prof. Siza D. Tumbo
KAIMU KATIBU MKUU
 
Hivi wakati anatoa taarifa za kukanusha ya Moshi/Kilimanjaro, Je yeye alikuwa Dar ama Dodoma na amekaa kwenye kiti cha kuzunguka ndani ya ofisi yenye kiyoyozi ..??
Nilidhani waziri alipaswa aende kwanza eneo la tukio ambapo imetokea tetesi ili akajiridhishe na wataalamu wake na baada ya hapo ndipo atowe tamko la kukanusha tetesi hizo akiwa yupo hukohuko Moshi/Kilimanjaro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri viongozi wa dini waanzishe dua na sala maalum ili Mungu atuepushe na hili balaa la nzige. Kama wanaomba wakati wa ukame hata kwa hili wanaweza kuomba.

Ikitokea nzige wakaharibu mazao yaliyobaki baada ya mengine kusombwa na mafuriko, Tanzania tutakuwa na njaa mbaya sana.
 
Salama!

Nilimsikia Waziri Hasunga akieleza jinsi walivyojipanga kupambana na nzige na hivyo wamekaa mkao tayari wa kuwasubiria!

Hili lilinishangaza kidogo.

Nzige wako umbali wa kilometer 50 kutoka mpaka wa Tanzania. Kwanini tusiunganishe nguvu na Wakenya tukapambana kuzuia wasiingie kwetu?

Lazima tuwasubirie waingie kwetu, watawanyike kisha ndio tuanze kuhangaika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa kilimo amekanusha tetesi hizi, binafsi naona kama amekalia kuti kavu na msaidizi wake nae anamuangalia tu ili akosee kisha atumbuliwe na kisha yeye msaidizi apande cheo na kuwa kamili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
beth,
awa Nzige badala ya kwamba tungekuwa tumeenda kusaidiana na wa-Kenya kuwatokomeza ama kuwasukuma waende mbali zaidi kule walikotokea, tunasubiri mpaka wapite Kenya waje Tanzania, halafu na sisi ndiyo tuanze kushughulika nao, kitu ambacho hatutaweza tena. Kama sasa hivi wako Kenya, na ikitokea wakawashinda wa-Kenya wakavuka hadi Tanzania, maana yake ni kwamba watakuwa wameshindikana,

Na itakuwa hakuna tena namna ya kuweza kuwaondoa. Tulitakiwa sasa hivi tuwe tuko Kenya tunashighulika nao kama tahadhari ya kuwafanya wasifike kwetu. Janga likishafika kwa jirani, husubiri mpaka lifike nyumbani kwako ndiyo uanze kushughulika nalo! Corona iko China lakini tahadhari kila mahali ni 100%.
 
Paul Alex,
Issue ya vifaranga bado inauma, Sisi tusubiri wafike wanakuja bado 50km waingie Mwanga ndiyo tuanze.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom