Serikali yatoa muongozo wa mitihani ya kitaifa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Picha

BARAZA la Mitihani la Tanzania, katika, litafanya upimaji wa kitaifa na kuendesha mitihani kwa watahiniwa wa madarasa mbalimbali, kikiwemo kidato cha sita chenye watahiniwa 90,182 katika mwaka wa fedha 2020/21.

Pia katika mwaka huo, Baraza litaendesha mtihani wa kidato cha Nne kwa watahiniwa 495,207 mwishoni mwa mwaka huu 2020.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wiziri wa Wizara hiyo, Profesa Joyce Ndalichako Ijumaa, Aprili 23, mwaka huu alisema, Baraza hilo litaendesha upimaji wa wanafunzi darasa la nne, la saba na kidato cha pili, nne na kidato cha sita mwaka wa fedha 2020/21.

Profesa Ndalichako alisema Baraza hilo litafanya upimaji kwa wanafunzi wa darasa la nne wapatao 1,825,387 na litaendesha mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa watahiniwa 1,009,938 kote nchini.

Pia Baraza hilo litaendesha upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili kwa watahiniwa 612,745. Pia litaendesha mtihani wa maarifa kwa watahiniwa 15,044 sambamba na kuendesha mitihani ya ualimu katika ngazi ya astashahada na stashahada kwa watahiniwa 8,135.

Pia litaendesha upimaji wa kitaifa wa umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa sampuli ya watahiniwa 33,350 wa darasa la pili Januari, 2021.

Vilevile, Waziri Ndalichako alisema Wizara hiyo imetoa ufadhili wa wahadhiri 620 kwa ajili ya kusoma masomo ndani na nje ya nchi.

Kati yao, wahadhiri 196 wanasoma shahada ya uzamili na wahadhiri 424 wanasoma shahada ya uzamivu kwa lengo la kuongeza idadi yao katika kutoa elimu katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu.

Pia wizara hiyo katika mkakati wa Mapinduzi ya nne ya viwanda nchini, imeanzisha mfumo wa kufundisha kozi mbalimbali katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Chuo Cha Sayansi cha Nelson Mandela Arusha na Chuo cha Ufundi Mbeya.

Vyuo vyote hivyo vimeanzisha kozi za kuhusu mapinduzi ya viwanda ili kusukumba mbele katika kufikia azma ya kuwa nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Wakati huo huo, Profesa Ndalichako amesema, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania katika mwaka wa fedha 2020/21,itakagua Vyuo Vikuu 25 kwa lengo la kuhakiki ubora wake.

Alisema pia itafanya tathmini ya programu 200 za masomo mbalimbali katika Vyuo Vikuu nchini na kuzisajili zile zitakazokidhi vigezo na itafanya tathmini na kutambua tuzo 5,000 zilizotolewa katika vyuo vikuu nje ya nchi.

Profesa Ndalichako amesema, itaratibu udahili na kuhakiki maombi ya wanafunzi takribani 100,000 wa mwaka wa kwanza watakaoomba kudahiliwa katika vyuo vya elimu ya juu katika programu mbalimbali.

“Itaandaa miongozo ya ulinganifu kwenye programu za masomo ya Uhandisi na Sayansi ya Tiba ya Binadamu,” alisema.

Pia alisema, itafanya utafiti ili kuweza kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali yenye lengo la kufanya maboresho kwenye mfumo wa utoaji elimu ya juu nchini.

Chanzo: HabariLeo
 
Rais Magufuli atakumbukwa kwa kuwalipia wanafunzi ada Tanzania nzima

Baaada ya miaka kumi tutakuwa na wanafunzi million kumi na tano waliopewa elimu bure na Magufuli
Usisahu na haya:
1. Atakumbukwa kwa kubariki makato ya 15% ya Heslb iliyopitishwa kibabe bila kuzingatia sheria na mkataba wa mkopo ambao ulitaka makato yawe 8% ya mshahara wa mnufaika.

2. Atakumbukwa kwa kukataa kujali maslahi ya watumishi wa umma
3. Mengine unayajua....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaratibu ni kama ifuatavyo:-
1: Nawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni (si chini ya sec 20) au tumia kitakasa mikono.
2: Epuka mambo yafuatayo:-
A:Kujishika usoni
B:Kushikana mikono na watu.
C:Kukaa sehemu zenye mikusanyiko.
3:Baki nyumbani kama huna safari ya lazima
4:Endapo utalazimika kutoka nyumbani vaa barakoa.
 
Yaani kubwabwaja kote huko hajaongelea kama mitiahani itafanyika September (std 7) ,November (form 2 & 4) na May (form 6) kama kawaida au itabidi isogezwe mbele kwasababu ya janga la Corona? Mhe.Waziri anakwama wapi?

Ukisoma mwaka wa fedha tajwa hapo juu ni dhahiri itafanyika baada ya mwezi wa saba.
 
Yaani kubwabwaja kote huko hajaongelea kama mitiahani itafanyika September (std 7) ,November (form 2 & 4) na May (form 6) kama kawaida au itabidi isogezwe mbele kwasababu ya janga la Corona? Mhe.Waziri anakwama wapi?
Mkuu we ndo hujamwelewa anamaanisha vyuo na shule vinaweza kufunguliwa kuanzia mwezi wa 8 maana mwaka wa fedha ni kuanzia mwezi wa 7 kama sijakosea
 
Rais Magufuli atakumbukwa kwa kuwalipia wanafunzi ada Tanzania nzima

Baaada ya miaka kumi tutakuwa na wanafunzi million kumi na tano waliopewa elimu bure na Magufuli
Kweli kabisa ...na amefanya vizuri kua wananchi kwasasa awalipi kabisa kodi
 
Mkuu we ndo hujamwelewa anamaanisha vyuo na shule vinaweza kufunguliwa kuanzia mwezi wa 8 maana mwaka wa fedha ni kuanzia mwezi wa 7 kama sijakosea
Acha masihala mzee yani mashule yafunguliwe had I mwezi wa 7 au 8 sasa wanafunzi wenyewe si watarudi na mimba wote
 
Usisahu na haya:
1. Atakumbukwa kwa kubariki makato ya 15% ya Heslb iliyopitishwa kibabe bila kuzingatia sheria na mkataba wa mkopo ambao ulitaka makato yawe 8% ya mshahara wa mnufaika.

2. Atakumbukwa kwa kukataa kujali maslahi ya watumishi wa umma
3. Mengine unayajua....

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wewe hata kama hauna akili sawa sawa, unashindwa kutumia hata tako kufikiria..... Hauoni amefanya jambo zuri kwa taifa, deni lolote ni lazima kulipwa..... Usipolipa mzigo watabeba wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli atakumbukwa kwa kuwalipia wanafunzi ada Tanzania nzima

Baaada ya miaka kumi tutakuwa na wanafunzi million kumi na tano waliopewa elimu bure na Magufuli
Usihau na hili
1. Atakumbukwa kwa kauli zake zinazochengana na maelezo yake
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom