Miss South Africa, Zozibini Tunzi ashinda taji la Miss Universe

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,822
4,603
IMG_3010.JPG

Miss Universe 2018 Catriona Gray kutoka Ufilipino akimvalisha taji mshindi mpya kutoka South Africa katika mashindano yaliyofanyika Desemba 8, 2019 Atlanta Marekani ndani ya Studio za Tyler Perry zilizozinduliwa hivi karibuni.

Warembo kutoka South Africa, Mexico na Puerto Rico waliingia tatu bora ambapo Zozibini Tunzi amechukua taji na Madison Anderson wa Puerto Rico amechukua nafasi ya pili.


Tunzi aliufurahisha umati wa waliohudhuria kwa kuzungumzia umuhimu wa uongozi kwa wanawake.

“Nafikiri moja ya vitu muhimu vya kuwafundisha wasichana leo ni uongozi. Ni kitu kinachokosekana kwa wanawake na wasichana kwa muda mrefu si kwa sababu hatutaki lakini ni kutokana na mifumo ya jamii.

Naamini sisi ni viumbe wenye nguvu zaidi duniani na tunastahili kila fursa. Na hiki ndicho tunachopaswa kuwafundisha wasichana, kuchukua nafasi. Hakuna kitu muhimu kama kuchukua nafasi kwenye jamii.”

Hii ni mara ya 3 kwa Afrika Kusini kushinda taji hili ambapo walishinda kwa mara ya kwanza mwaka 1978 na kushinda tena 2017.
 
Kazuri....Ila yule wa Angola aisee😍😍😋😋
 
Back
Top Bottom