Lipumba ashinda Uenyekiti wa CUF kwa asilimia 88

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Napokea taarifa rasmi kuwa, Leo Profesa Ibrahim Lipumba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CUF kwa kupata kura 516 sawa na asilimia 88.

#Note Naweza kusema kuwa, leo CUF imekamilisha hatua ya mwisho iliyokuwa imebakia ili ikamilike kuwa kama NCCR, TLP, UDP.
=====

Profesa Ibrahim Lipumba ameshinda nafasi ya uenyekiti wa CUF Taifa.

Lipumba ameshinda leo Machi 13, 2019 kwenye uchaguzi mkuu wa saba wa chama hicho uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Akitangaza majina ya washindi katika uchaguzi huo, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Thenei Ally Juma amesema Lipumba amepata kura 516 sawa na asilimia 88.9.

Hata hivyo, haikuelezwa ni kura ngapi zimepigwa. Lakini ukumbi ulikuwa na jumla ya wajumbe 598.

Amemtaja aliyeshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuwa ni Maftaha Nachuma aliyepata kura 231 sawa na asilimia 40.9.

Juma amemtangaza pia Abbas Juma Muhunzi kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar baada ya kupata kura 349 sawa na asilimia 60.9.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Profesa Lipumba amesema walioshinda ni vijana wake na hana tabu nao.

“Nitafanya nao kazi, wengi wao wameulizwa kushika nafasi hizo jana na leo wameshiriki na wameshinda,” amesema Lipumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila CUF wanajuta kutumreplace Lipumba Mapema.Sasa ndo kawa rasmi mwenyekiti baada ya kujiondoa na kurudi tena.Katibu mkuu bado ni Maalim Seif.Hapa cha muhimu waweke tofauti zao pembeni na wafanye kazi kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Napokea taarifa rasmi kuwa, Leo Profesa Ibrahim Lipumba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CUF kwa kupata kura 516 sawa na asilimia 88.

#Note Naweza kusema kuwa, leo CUF imekamilisha hatua ya mwisho iliyokuwa imebakia ili ikamilike kuwa kama NCCR, TLP, UDP.

Sent using Jamii Forums mobile app
Li-pumba pandikizi la ccm mgogoro wake na CUF Maalim Seif hautaisha ni kama wapalestina na waizrael
 
Ila CUF wanajuta kutumreplace Lipumba Mapema.Sasa ndo kawa rasmi mwenyekiti baada ya kujiondoa na kurudi tena.Katibu mkuu bado ni Maalim Seif.Hapa cha muhimu waweke tofauti zao pembeni na wafanye kazi kama ilivyokuwa mwanzo.

Huyo Maalim Seif kesho anapigwa chini, mwenyekiti ata_propose majina mawili ambayo yatapigiwa kura kuchagua katibu mkuu mpya.
 
Na hiyo ndio ilikuwa timing nzuri, shida ilikuja pale ambapo walipoingia kwenye mgogoro mapema na kuacha kiti wazi. All in all hata huo ni u dictator,
 
Huyo Maalim Seif kesho anapigwa chini, mwenyekiti ata_propose majina mawili ambayo yatapigiwa kura kuchagua katibu mkuu mpya.
Maalifu Seif kajimaliza na sumu aliyoiweka mwenyewe kwaajili ya kuwaua kina Mzee Mapalala na Shaban Mloo, kwa bahati mbaya hakufahamu maana vikombe vilifanana kaangukia kunywa kikombe kilekile akidhani hakina sumu.
 
Napokea taarifa rasmi kuwa, Leo Profesa Ibrahim Lipumba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CUF kwa kupata kura 516 sawa na asilimia 88.

#Note Naweza kusema kuwa, leo CUF imekamilisha hatua ya mwisho iliyokuwa imebakia ili ikamilike kuwa kama NCCR, TLP, UDP.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka kwamba kuna kesi mahakamani hukumu machi 18
 
Ila CUF wanajuta kutumreplace Lipumba Mapema.Sasa ndo kawa rasmi mwenyekiti baada ya kujiondoa na kurudi tena.Katibu mkuu bado ni Maalim Seif.Hapa cha muhimu waweke tofauti zao pembeni na wafanye kazi kama ilivyokuwa mwanzo.
Seif akiweka pembeni tofauti zake na Lipumba basi hawezi kubaki Seif yuleyule, atakuwa sawa na Mrema na Cheyo.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom