Baba matatani kwa kumfinya akitumia praizi mtoto kisa hajui kusoma wala kuandika

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,325
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanaume aitwaye Shija Abdallah (28), mkazi wa kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga kwa kosa la kumshambulia kwa kumfinya kwa kutumia Praizi mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 8 anayesoma darasa la tatu katika shule ya msingi Kambarage.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo Januari 15, 2021 saa majira ya saa nane kamili mchana.

“Tunamshikilia Shija Abdallah kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili baada ya kumfinya kwa kutumia praizi mwanae wa kiume, (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 08, mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kambarage sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Bibi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa kata ya Ndala, Manispaa ya Shinyanga alibaini mtoto huyo kufanyiwa ukatili huo na baba yake mzazi huyo kwa kufinywa kwa kutumia praizi sehemu mbalimbali za mwili wake chanzo kikiwa ni kumuadhibu mtoto huyo kwa sababu hajui kusoma wala kuandika na mahudhurio shuleni ni hafifu”,amefafanua Kamanda Magiligimba.

Amesema madhura amepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na hali yake inaendelea vizuri na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

“Natoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wao na watumie njia sahihi ya kuwaadhibu watoto pindi wakoseapo.

“Jeshi la polisi mkoani Shinyanga halitamvumilia mzazi au mlezi yeyote atakayebainika kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake na niwatake wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kukomesha vitendo hivi vya ukatili dhidi ya watoto”,amesema.
 
Inawezekena mtoto ni dyslexie, hili jambo linatakiwa kuelimishwa kwa umma.

Mtoto anapokua dyslexie anakua na matatizo ya kusoma na kuandika ila kuna namna ya kumfundisha taratibu na akaelewa. Watoto wa namna hii wanahitaji kuwa karibu na mwalimu.

Kwa madarasa yetu yenye watoto 80, mwalimu hawezi kukumbuka majina ya wanafunzi wote atapataje muda wa kumsaidia mtoto mwenye dyslexie.
 
Huyo mzee anahisi mtoto ni mzembe masikini. Ila haelewi kuwa tumetofautiana capacity ya ku master vitu. Wengine ni slow learners inachukua mda ku grasp a piece of knowledge.

After all that being said kumpiga mtoto sio solution. Nakumbuka mshua alikuwa ananitia makonzi na yeye ndie alinifundisha kusoma baada ya kuninunulia kitabu cha soma kwa hatua. 😂😂😂 Alinifumua ila nilifanikiwa kuelewa kusoma na kuandika very fast. Tukimaliza kusoma ananipe hela ya pipi.

Nilijua kusoma gazeti vizuri kabisa by the time i am 7 yrs! Nimeanza shule najua kuandika na kusoma kabisa.
 
Huyo mzee anahisi mtoto ni mzembe maskini. Ila haelewi kuwa tumetofautiana capacity ya ku master vitu. Wengine ni slow learners inachukua mda ku grasp a piece of knowledge.

After all that being said kumpiga mtoto sio solution. Nakumbuka mshua alikuwa ananitia makonzi na yeye ndie alinifundisha kusoma baada ya kuninunulia kitabu cha soma kwa hatua. 😂😂😂 Alinifumua ila nilifanikiwa kuelewa kusoma na kuandika very fast. Tukimaliza kusoma ananipe hela ya pipi.

Nilijua kusoma gazeti vizuri kabisa by the time i am 7 yrs! Nimeanza shule najua kuandika na kusoma kabisa.
Ndo kina Diamond wajao hawa, issue moja skuli nakumbuka kuna msela Gerald tulikua tunavizia kidemu Mgeni kimbulu hivi cheupeee.

Mi na jamaa tukachapana sana mingumi mpirani huko kisa hakijulikani.

Badae nakuja kujua kumbe anamind nakaa na wale watoto dawati moja na Mgeni na Asunta,

Kichekesho sasa Asunta alikua black beauty na ana chura balaa,ki mgeni kipo tu kinapepesuka.

Jamaa Gerald aliweka fitna siku akaandika barua ya mapenzi kaweka jina langu.

Akaangusha barua njia ya kwenda ofisini kwa walimu.

Imeokotwa ikapelekwa ofisini nilipigwa viboko na walimu wote.

Mama yangu nae mwalimu hapohapo nae kanichapa mbaya.akaondoka na hiyo barua kaipeleka home kwa mdingi.

Mdingi nae katoka kwa mchepuko siku mbili hakuwa home, aisee nilipigwa mimi, mdingi anafukia mashimo nikaninginizwa juu ya dari nimenyongwa kwa taulo mpk nakaribia kukata kauli ndo kanishusha alafu kanisindikiza na teke kali sana(toka siku hiyo sikulala nyumbani)

Niliomba ukimbizi kwa aunt mjini huko walinipata baada ya siku 2.hakukua na cm enzi hizo
 
Mshua boi angekuua huyo 😂😂😂 hii ndo shida ya kuwa na baba mwanajeshi😝
 
Inawezekena mtoto ni dyslexie, hili jambo linatakiwa kuelimishwa kwa umma.

Mtoto anapokua dyslexie anakua na matatizo ya kusoma na kuandika ila kuna namna ya kumfundisha taratibu na akaelewa. Watoto wa namna hii wanahitaji kuwa karibu na mwalimu.

Kwa madarasa yetu yenye watoto 80, mwalimu hawezi kukumbuka majina ya wanafunzi wote atapataje muda wa kumsaidia mtoto mwenye dyslexie.

Nimefurahi sana kuona komenti yako ulivyogusa hilo eneo na kitaalamu inaitwa specific learning difficulties ambapo yapo makundi matatu msingi

Dyslexia (kusoma)
Dysgraphia (kuandika)
Dyscalculia (kuhesabu)

Ndio maana tunashauri walimu wa elimu maalumu ndio wawe walimu wa kufundisha madarasa ya awali ili wawahi changamoto hizo zikiwa bado mapema.

Nitafundisha darasa la kwanza somo la kusoma na kuandika ili tusaidie taifa katika hilo

Mwl wa akiba
 
Kumbee kipindi kikee Digi alivyo kuwa ananiazibu vile ingekuwa Sasa angepata kesi, alikuwa Ana tuingiza kwenye gunia Yale ya katani, anaweka majani ya washawasha analifunga kwenye paa ya nyumba then anaanza kukulamba bakoraa asee we achaa tu. Ila kiasi flani ilinirudisha kwenye njia.
 
Ndo kina Diamond wajao hawa, issue moja skuli nakumbuka kuna msela Gerald tulikua tunavizia kidemu Mgeni kimbulu hivi cheupeee.

Mi na jamaa tukachapana sana mingumi mpirani huko kisa hakijulikani.

Badae nakuja kujua kumbe anamind nakaa na wale watoto dawati moja na Mgeni na Asunta,

Kichekesho sasa Asunta alikua black beauty na ana chura balaa,ki mgeni kipo tu kinapepesuka.

Jamaa Gerald aliweka fitna siku akaandika barua ya mapenzi kaweka jina langu.

Akaangusha barua njia ya kwenda ofisini kwa walimu.

Imeokotwa ikapelekwa ofisini nilipigwa viboko na walimu wote.

Mama yangu nae mwalimu hapohapo nae kanichapa mbaya.akaondoka na hiyo barua kaipeleka home kwa mdingi.

Mdingi nae katoka kwa mchepuko siku mbili hakuwa home, aisee nilipigwa mimi, mdingi anafukia mashimo nikaninginizwa juu ya dari nimenyongwa kwa taulo mpk nakaribia kukata kauli ndo kanishusha alafu kanisindikiza na teke kali sana(toka siku hiyo sikulala nyumbani)

Niliomba ukimbizi kwa aunt mjini huko walinipata baada ya siku 2.hakukua na cm enzi hizo
Asunta kama Asumpta 😄😄😄😄😄🤣
 
Huyo ni baba ako? Muulize mamako vizuri babab ko atakuwa nyange
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom